Mhariri wa Radio Times 100.5 FM, Bw. Mkombe Zanda, akitoa maelezo kwa Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Kamishna Msaidizi, Bw. Abdallah Mssika, namna uzalishaji wa vipindi, matangazo na kazi nyingine za kurekodi sauti zinavyofanyika kwenye chumba cha uzalishaji (Production Room) wakati wa ziara yake kwenye studio zetu.
Sunday, February 22, 2009
Ziara ya Kamanda Mssika Radio Times 100.5 FM
Saturday, February 7, 2009
Hafla ya kumuaga Mama Nyaulawa
Friday, February 6, 2009
Mugabe kusaini mabadiliko ya katiba
HARARE,
RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe, anatarajiwa kusaini mabadiliko ya sheria kwenye katiba ya nchi hiyo yatakayomwezesha Kiongozi wa Upinzani kutoka chama cha Movement for Democratic Change, MDC, Bwana Morgan Tsvangirai, kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Serikali hiyo inaundwa kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa kugawana madaraka baina ya chama tawala Zanu-PF na kambi ya upinzani Septemba 15 mwaka jana ikiwa ni hatua ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Baada ya Rais Mugabe kusaini mabadiliko hayo, Bwana Tsvangirai, anatarajiwa kuapishwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Zimbabwe Jumatano, Februari 11 mjini Harare.
Mabadiliko hayo yamepitishwa hivi karibuni na bunge la Zimbabwe na kutoa nafasi kwa viongozi hao kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hata hivyo, baadhi ya nchi hisani zikiwemo Marekani na Uingereza pamoja na Umoja wa Ulaya zimeweka wazi misimamo yao kuwa hazitaondoa vikwazo vyao kwa Zimbabwe hadi hapo Serikali hiyo itakapotimiza lengo la kuundwa kwake.
Rais Somalia aomba suluhu na al-Shabaab
ADDIS ABABA,
RAIS mpya wa Serikali ya mpito ya Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ameonesha nia ya kufanya mazungumzo na kundi la al-Shabaab linaloshikilia maeneo mengi muhimu ya nchi hiyo na kuisababisha Serikali yake kushindwa kufanyakazi nchini humo.
Viongozi wa Serikali hiyo hivi sasa wanaishi kwenye nchi za Kenya na Djibouti baada ya kundi hilo kuuteka mji wa Baidoa uliokuwa ukitumiwa na Serikali hiyo kama makao yake makuu.
Sheikh Sharif, amesema njia pekee ya kuleta umoja na mshikano nchini humo na hatimaye kurejesha amani ya Somalia ni kwa Serikali yake kufanya mazungumzo na kundi la al-Shabaab.

Amesema, Somalia kwa sasa inakabiliwa wa ukosefu wa umoja miongoni mwa raia wake huku kila mmoja akidhani kuwa ana haki ya kufanya mambo nchini humo bila ya kuwashirikisha wengine jambo ambalo amesema sasa linapaswa kuondolewa na kujenga Somalia moja.
Sheikh Sharif, alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Umoja wa Mahakama za Kiislam ulioshika madaraka kwa takriban miezi sita kabla ya utawala wao kuondolewa madarakani na majeshi ya Ethiopia na amechaguliwa hivi karibuni na bunge la nchi hiyo kuchukua nafasi ya Rais Abdillah Yusuf Ahmed, aliyejiuzulu Disemba mwaka jana.
Chenge ni Shujaa !?

Mafunzo ya Tovuti kwa Wahariri
WAHARIRI wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wamepatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya tovuti mbalimbali kwa ajili ya shughuli zao za kuhariri habari.
Mafunzo haya yameandaliwa na MISA Tanzania na yameendeshwa na Mkufunzi kutoka Shirika la Utangazaji la Finland, Bwana Peik Johansson, yamefanyika kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM, jijini Dar es Salaam.
MHARIRI wa Radio Times 100.5 FM,
Mafunzo haya yameandaliwa na MISA Tanzania na yameendeshwa na Mkufunzi kutoka Shirika la Utangazaji la Finland, Bwana Peik Johansson, yamefanyika kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM, jijini Dar es Salaam.

Bw. Mkombe Zanda, (kushoto) akiwa kwenye mafunzo hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)