Sunday, February 22, 2009

Ziara ya Kamanda Mssika Radio Times 100.5 FM

Mhariri wa Radio Times 100.5 FM, Bw. Mkombe Zanda (kulia) akitoa maelezo kwa Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Kamishna Msaidizi, Bw. Abdallah Mssika, wakati alipotembelea studio zetu Mtaa wa Lugoda, Kariakoo, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamu shughuli zetu na kuboresha uhusiano baina ya kituo chetu na jeshi la polisi. Katikati ni watangazaji wa Radio Times, Suleiman Semunyu na Michael Saduka (aliyevaa fulana nyeusi)

Mhariri wa Radio Times 100.5 FM, Bw. Mkombe Zanda, akitoa maelezo kwa Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Kamishna Msaidizi, Bw. Abdallah Mssika, namna uzalishaji wa vipindi, matangazo na kazi nyingine za kurekodi sauti zinavyofanyika kwenye chumba cha uzalishaji (Production Room) wakati wa ziara yake kwenye studio zetu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Kamishna Msaidizi, Bw. Abdallah Mssika, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali za kampuni ya Business Times kwenye ofisi za kampuni hiyo mtaa wa Lugoda, Kariakoo jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment