Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Times 100.5 FM, Bw. Rehure Nyaulawa (wa pili kulia) akigonganisha glasi na Mama yake mzazi, Bibi. Getrude Nyaulawa (kushoto) aliyekuwa Meneja Mkuu wa BPL katika hafla ya kumuaga baada ya kustaafu kazi.
Radio Times 100.5 Fm inarusha matangazo yake katika masafa ya 100.5 FM na inasikika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Morogoro,Zanzibar na maeneo mengine ya jirani ambayo matangazo ya radio Times yanafika.
Ikiwa ni chombo cha habari, Radio Times ina jukumu la kuwahabarisha wananchi mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na nje ya mipaka ya Tanzania, kuwaburudisha na kuwaelimisha kuhusu masuala mbalimbali ya kiburudani, kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Inapendeza kwa kweli naomba muiboreshe ndugu zangu. Anita Kiteni, Moro
ReplyDelete